Habari za Punde

*WAREMBO WA DAR CITY CENTER WAJIFUA KUJIANDAA NA SHINDANO LAO LA MEI 13

Jumla ya Warembo 18, wameanza mazoezi ya pamoja katika Ukumbi wa Hoteli ya Lamada Ilala Dar es Salaam jana kwa ajili ya kujiandaa na shindano la kumsaka Miss Dar City Center 2011, linalotaraji kufanyika kwenye Ukumbi huo huo Tarehe 13 mwezi wa tano mwaka huu. Warembo hao wakiwa katika mazoezi ya kudansi.
Mazoezi ya kutembea 'Cat Walk'...
Hawa ndiyo warembo 18, wanaotarajia kushiriki katika kinyang’anyiro cha kumsaka Miss Dar City Center 2011, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazoezi yao ya kujiandaa na shindano hilo linalotarajia kufanyika Mei 13 mwaka huu katika Ukumbi wa Hoteli ya Lamada Ilala Dar es Salaam.
Hizi ni baadhi ya Pozi za picha kutafuta nani mkali anaweza kuibuka katika Kategoli ya 'Photo Genic'
Pozi Baaab Kubwa......
Si doli la dukani bali ni pozi la picha....
Si Studio hapa bali ni pozi la photoo!....
Huyu hajalazimishwa wala kufundishwa pozi hili amepozi mweeeeenyewe!
Si kwamba anaogopa kamera la hasha, bali ni pozi tofauti la kivyake, inaelekea utotoni aliupenda sana mchezo wa kujificha!...
Nani Mkali wa ozi kati ya hawa??? Yeeees! Pozi la pmoja limenoga hapa.....Nani kamuiga mwenzie hapa??

Baadhi ya wachezaji wa timu ya Simba, wakiwa katika ukumbi wa Hoteli ya Lamada Ilala juzi, wakiangalia mazoezi ya warembo hao.
Baadhi ya warembo waliowahi kushiriki katika mashindano hayo yaliyopita wakiwa ukumbini humo kuangalia mazoezi hayo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.