Wachezaji wa Yanga, wakishangilia moja ya bao lililofungwa na Idd Mbaga, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliochezwa jioni hii kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 3-1, ambapo magoli 2 yamefungwa na Idd Mbaga na moja likifungwa David Mwape, kwa ushindi huo sasa Yanga imerejea kukaa kileleni baada ya kuwa na Pointi 46 sawa na watani wao wa Jadi Simba, kwa hatua hiyo Utofauti wa magoli ya kufunga na kufungwa ndiyo unaangaliwa ambapo Simba amefunga 36 na kufungwa 15, huku Yanga akifunga 29 na kufungwa 7. Golikipa wa African Lyon, Ivo Mapunda akijaribu kuokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni kwake, wakati wa mchezo huo.
Kuanzia Januari 2025, vivuko vitakuwa vinasubiria abiria, Sea Tax kuongezwa
Dar: Bashungwa
-
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa Serikali kupitia Wakala
wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa kushirikiana Kampuni ya Azam Marine
zinaendele...
27 minutes ago
No comments:
Post a Comment