Habari za Punde

*FIESTA YAZINDULIWA NA BONANZA LA MASHABIKI WA TIMU ZA SOKA ZA ULAYA

Mashabiki wa timu ya Manchester United, wakishangilia na kuimba wimbo wao baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni leo, wakati wa Uzinduzi wa Fiesta, iliyozinduliwa kwa staili ya kuwashirikisha mashabiki wa timu za Soka za Ulaya ambapo walishiriki katika Bonanza la pamoja kwa kucheza mechi, pamoja na burudani nyingine.
Gari la Clouds Fm, likiwa kwenye viwanja hivyo kwa ajili ya kurusha live mambo yaliyokuwa yakijili katika viwanja hivyo.
Maandamano ya mashabiki hao yalianzia kwenye Viwanja vya Biafra Kinondoni hadi Leaders kama hivi.
Kipa wa timu ya Mashabiki wa Man U, akipotea maboya wakati wa hatua ya kupigiana penati kati ya Man U na Real Madrid, ambapo Madrid ilishinda kwa mikwaju ya penati.
Mchezaji wa timu ya mashabiki wa timu ya Chelsea, Samuel Temi, (ushoto) akipiga mpira wakati akichuna na mpinzani wake beki wa Liver Pool, Boniface Pawasa, wakati wa mchezo wa timu za Mashabiki wa timu za Ulaya, uliochezwa kwenye Viwanja vya Leaders Club leo, ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Tamasha la Fiesta linalotarajia kuanza hivi karibuni. Chelsea ilishinda 2-0.
Jerry Tegete (kulia) na Clement Kaabuka (katikati) wakiruka kwa pamoja kumdhibiti mpinzani wao, wakati wa mchezo huo.
Ibrahim Maestro wa Man U (kushoto) akijaribu kupiga mpira mbele ya beki wa Real Madrid, wakati wa mchezo wao. Madrid ilishinda kwa mikwaju ya penati.
Nyanda wa Man U (kushoto) akiambaa na mpira.
Kikosi cha timu ya Mashabiki wa Chelsea, kabla ya kuanza mtanange huo.
Kikosi cha timu ya Mashabiki wa Liver Pool, kabla ya kuanza mtanange huo.
Mashabiki wa AC Milan, wakiimba wimbo wao wakati wa mapokezi ya timu hizo.
Mashabiki wa Madrid, wakiserebuka na wimbo wao.
Mashabiki wa Man U wakifurahia kwa mbwembwe.
Mashabiki wa Chelsea, wakiimba wimbo wao.
Unkal Michuzi akijumuika na mashabiki wenzake wa Liver Pool, kuimba wimbo wao.
Mashabiki wa Arsenal, wakiimba wimbo wao.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.