Habari za Punde

*MKE WA MUBARAK AKABIDHI MALI ZAKE KWA MISRI

Mke wa rais wa Misri, Hosni Mubarak, aliyeondolewa madarakani, ambaye alikuwa akishikiliwa kwa makosa ya ulaji rushwa, ameachiwa kwa dhamana baada ya kukabidhi mali zake.

Maofisa walisema kuwa mkewe, Suzanne Mubarak, alikabidhi nyumba ya kifahari iliyopo kwenye kitongoji cha mjini Cairo na fedha zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 3 zilizoshikiliwa kwenye akaunti mbalimbali za benki nchini Misri.


Familia ya Bw Mubarak inakabiliwa na madai ya "kupata mali kinyume cha sheria" wakati alipokuwa madarakani kwa miaka 30.


Bw Mubarak aliyeondoshwa madarakani mwezi Februari pia anashutumiwa kuhusika katika mauaji ya waandamanaji waliopinga uongozi wake.


Watoto wake wawili wa kiume, Alaa na Gamal, kwa sasa wanashikiliwa kwenye gereza la Tora kwa makosa ya udanganyifu.




No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.