Habari za Punde

*MTETEZI WA MAPENZI YA JINSIA MOJA AUAWA

Wapenzi wa jinsia moja

Mauaji ya kikatili ya mwanaharakati wa kutetea mapenzi ya jinsia moja kutoka Afrika kusini yamelaaniwa na kuelezwa kama uhalifu unaohusishwa na chuki na shirika la Human Rights Watch.


Shirika hilo lenye makao yake makuu nchini Marekani limewasihi polisi kufanya jitihada zaidi ya kuwapata waliohusika na mauaji ya hivi karibuni na ubakaji wa Noxolo Nogwaza.


Aliuliwa kwa kupopolewa na mawe na kuchomwa kisu Aprili 24 baada ya kutokea mabishano kwenye baa katika kitongoji cha KwaThema, mashariki mwa Johannesburg.


Wanaharakati wamesema wapenzi wa jinsia moja wa kike nchini humo hulengwa kwa kile walichosema "ubakaji wa kurekebishwa".


Tofauti na nchi nyingi za Afrika, mapenzi ya jinsia moja ni halali Afrika kusini na katiba inaharamisha ubaguzi kwa misingi ya jinsia yako.


Lakini wanaharakati wamesema wapenzi wa jinsia moja hushambuliwa kwenye vitongoji mbalimbali.


Polisi wamesema wanafanya uchunguzi juu ya mauaji hayo na wanasubiri matokeo ya uchunguzi wa maiti.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.