Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto)akisikiliza maelezo ya Elizabeth Mlay, mwanafunzi wa kidato cha sita shule ya Sekondari Jangwani iliyopo jijini Dar es Salaam, jinsi ya kutengeneza dawa ya kusafishia na kuondoa harufu chooni. Waziri Prof. Makame alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa sherehe za mwaka wa kimataifa wa kemia zilizoandaliwa na Chama cha wakemia Tanzania kwa kushirikiana na Kamisheni ya Taifa ya UNESCO uliofanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Picha na Anna Nkinda – Maelezo
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akimshauri Mkuu wa kitengo cha Kemia kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam Dk. Phillip Joseph jinsi gani wanaweza kufanya kazi ya kuchuja maji hadi kufikia hatua ya kuwa maji safi na salama.
No comments:
Post a Comment