Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi, akizungumza na wasanii wa sanaa za ufundi, maonyesho na picha nyongefu (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa kazi zao kwa jamii katika ukumbi wa mikutano wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ilala jijini Dar es Salaam leo. Picha na Anna Nkinda-MAELEZO
Muigizaji wa picha nyongefu, Hemedi Maliyaga, maarufu kama “Mkwere” akijitambulisha jina lake mbele ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi (hayupo pichani) wakati waziri huyo alipokutana na wasanii wa sanaa za ufundi, maonyesho na picha nyongefu ili kujua matatizo yanayowakabili. Muigizaji wa picha nyongefu, Emmanuel Myamba, akimueleza Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi (hayupo pichani) jinsi ambavyo Serikali inakosa mapato kutokana na kazi za wasani.
Asha Salimu ambaye ni muongozaji wa filamu akimueleza Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi (hayupo pichani) umuhimu wa wasanii kupewa elimu zaidi ili waweze kufanya kazi zao vizuri. Waziri Dk. Nchimbi alikutana na wasanii wa sanaa za ufundi leo, maonyesho na picha nyongefu katika ukumbi wa mikutano wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ilala jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment