Habari za Punde

*JUMUIYA YA WACHINA WAISHIO NCHINI WASHEREHEKEA SIKU YA MTOTO DUNIANI KWA KUWAFARIJI WATOTO YATIMA WA KITUO CHA KURASINI DAR

Xu Wu (Kulia) kutoka Jumuia ya wachina waishio nchini Tanzania akiwakabidhi mikebe ya shule baadhi ya watoto kutoka kituo cha kulelea watoto Yatima cha Kurasini jijini Dar es Salaam. Wachina hao walitetembelea kituo hicho jana kwa ajili ya kusherehekea siku ya mtoto pamoja na watoto yatima na kuwapatia zawadi mbalimbali zikiwemo nguo, viatu, masanduku ya kuwekea nguo, vyakula, madawa na vifaa vya kuchezea. Picha na Anna Nkinda-MAELEZO Baadhi ya wachina kutoka Jumuia ya wachina waishio nchini Tanzania wakipozi na watoto wa kituo cha kulelea watoto Yatima cha Kurasini jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza kuwagawia zawadi.

Jumuia ya wachina waishio nchini Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na watoto pamoja na walezi kutoka kituo cha kulelea watoto Yatima cha Kurasini jijini Dar es Salaam. Wachina hao walitetembelea kituo hicho jana kwa ajili ya kusherehekea siku ya mtoto pamoja na watoto yatima na kuwapatia zawadi mbalimbali zikiwemo nguo, viatu, masanduku ya kuwekea nguo, vyakula, madawa na vifaa vya kuchezea. Yu Xiu Mei (kushoto) kutoka Jumuia ya wachina waishio nchini Tanzania akimkabidhi Margaret Mkandawire (kulia) ambaye ni Mkuu wa kituo cha kulelea watoto Yatima cha Kurasini jijini Dar es Salaam. Xu Wu (Kushoto) kutoka Jumuia ya wachina waishio nchini Tanzania akimkabidhi nesi Eulelia Michael (kulia) kutoka kituo cha kulelea watoto Yatima cha Kurasini jijini Dar es Salaam maboxi yenye dawa za kutibu ugonjwa wa maralia kwa watoto .

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.