Habari za Punde

*KOCHA WA TAIFA STARS JAN POULSEN KUKUTANA NA MAKOCHA 32 WA KLBU ZA LIGI KUU

TAARIFA kutoka Boniface Wambura Ofisa habari wa TFF alizozitoa kwa vyombo vya habari asubuhi hii zinadai kuwa Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen pamoja na Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Sunday Kayuni watakutana na makocha 32 wa klabu za Ligi Kuu na Daraja la Kwanza. Mkutano huo utafanyika Juni 20 mwaka huu Ofisi za TFF kuanzia saa 3 asubuhi.

Pamoja na mambo mengine, mkutano huo ni maalumu kwa Poulsen kueleza falsafa yake
ya ufundishaji, tathmini ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyomalizika Aprili mwaka huu,
kutoa leseni za daraja A za ukocha za TFF kwa makocha husika na kubadilishana
uzoefu.
Makocha husika wanatakiwa kugharamiwa na klabu zao kwa ajili ya kushiriki
mkutano huo muhimu. TFF itagharamia chai na chakula cha mchana pekee. Klabu za
Ligi Kuu ni African Lyon, Azam, Coastal Union, JKT Ruvu, Kagera Sugar, Moro
United, Mtibwa Sugar, Oljoro JKT, Polisi Tanzania, Ruvu Shooting, Simba, Toto
Africans, Villa Squad na Yanga.

U 23 v NIGERIA OLIMPIKI Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23 ambayo Jumamosi (Juni 18 mwaka huu) itacheza ugenini na Nigeria katika mechi ya marudiano ya mchujo kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki itakayofanyika mwakani London, Uingereza itaagwa kesho.

U 23 itaagwa saa 7 mchana kambini F&J Hotel iliyoko Mikocheni, Dar es Salaam.
Mechi dhidi ya Nigeria itachezwa Uwanja wa Samuel Obgemudia ulioko Benin City, ambapo ni kilometa 320 kutoka Jiji la Lagos.
Waamuzi wa mechi hiyo ambao wote wanatoka Senegal ni Ousmane Fall (mwamuzi wa kati), Maguette Ndiaye, Cheikh Toure na mwamuzi wa akiba Daouda Gueye. Kamishna ni Emmanuel Zombre kutoka Burkina Faso.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.