Habari za Punde

*MATUKIO YA UFUNGAJI WA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA SONGEA KATIKA PICHA

Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais, Terezya Luoga wa (katikati) akimkabidhi kikombe cha ushindi wa jumla mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa, Aman Mwamwindi (katikati mwenye kofia), baada ya Manisppaa hiyo kushika nafasi ya kwanza kitaifa kwa usafi, kushoto ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu katika maadhimisho ya siku ya mazingira ambayo kitaifa yalimalizika mjini Songea mkoa wa Ruvuma. Picha na Muhidin Amri,Songea

Mwanadada, Azara Challes (21) akionyesha umahiri wake wa kuchezea mpira kwa staili tofauti kwenye uwanja wa majimaji wakati wa kilele cha siku ya mazingira iliyofanyika mjini Songea Mkoani Ruvuma.


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka (kushoto) akiwakabidhi zawadi viongozi wa Wilaya ya Mpanda Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mpanda, Enock Gwambasa, (wa pili kushoto) Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt Rajabu Rutengu, ambayo ni ya ushindi wa kwanza kwa usafi.Picha ya pamoja baada ya shughuli hiyo.




No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.