Habari za Punde

*ONYESHO LA ‘FASHION 4 VISION’ LAKUSANYA MILIONI 15/=


Na Mwandishi Wetu, JIJINI
ONYESHO maalumu la mavazi llinalobeba ujumbe wa ‘Fashion 4 Vision’ lililofanyika mwishoni mwa wiki Dar es Salaam limechangisha sh. mil 15/- zitakazosaidia matibabu ya wagonjwa wa macho nchini.
Onyesho hilo liliandaliwa na Lions Club Tanzania chini ya uratibu wa Wabunifu wa Mavazi Mustapha Hassanali na Jamila Veraswai na kudhaminiwa na Benki ya Exim
Tanzania ambapo vitu mbalimbali yakiwemo mavazi ya mitindo tofauti yalinadiwa na mgeni rasmi Mama Salma Kikwete kwa waliohudhuria.
Akizungumzia onyesho hilo Mama Salma aliipongeza Lions Club pamoja na wabunifu Hassanali na Veraswai kwa kuwa na mawazo chanya ya kusaidia jamii ya kitanzania ambapo pia aliwashukuru na kuwapongeza wote waliojitokeza katika onyesho hilo na
kuchangia kutunisha mfuko kwa ajili ya matibabu ya wagonjwa husika.

“Ni mawazo yanayopaswa kuungwa mkono na mimi binafsi nawapongeza Lions pamoja na

wabunifu wetu kwa kuonyesha moyo wa imani kwa wenzetu wanaosumbuliwa na maradhi lakini niwapongeze pia waliojitokeza leo na kuchangia fedha”,alisema Mama Kikwete.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Benki ya Exim Dinesh Arora alisema pamoja na udhamini wamechangia sh.milioni moja katika mfuko huo na kwamba hiyo ni katika utekelezaji wa majukumu ya kawaida ya kibenki kwa jamii ya kitanzania wanaochangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa benki hiyo.

“Tumekuwa tunafanya biashara ya kibenki kama jukumu letu kuu lakini pia tumekuwa na majukumu mengine kwa jamii inayotuzunguka hivyo udhamini pamoja na mchango wetu katika hafla ya leo ni miongoni mwa utekelezaji wa majukumu hayo,” alisema Arora.

Rais wa Lions Club Frank Goyayi alisema hafla hiyo ilitarajiwa kukusanya sh. milioni 10/= lakini ni jambo la kutia moyo kuona wamevuka lengo na kwamba hiyo inawahakikishia kuwa watafanikiwa katika yale waliyoyalenga kwa wagonjwa wa macho nchini.

“Tumefarijika na kututia moyo kwa kiasi kikubwa na sasa tuna imani ya kufanikiwa katika yale tuliyoyalenga,tunawashukuru wote waliojitolea kudhamiani na kuchangia kwa moyo wao wa upendo kwa wenzao wanaosumbuliwa na maradhi,” alisema
Goyayi.




No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.