Makamu wa Rais, Dkt. Bilal na kewe Mama Zakia Bilal (wapili kulia) wakipiga picha ya kumbukumbu na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Haji Hamis na baadhi ya Wanachama wake, wakati walipofika katika hafla ya kukutana na watanzania waishio New York na Vitongoji vyake jana.
Sufianimafoto pia alikuwa ni miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo, hapa akipozi na mchezaji wa zamani wa timu ya Balimi Fc ya Kagera, Henri (wa pili kushoto) na dada zake.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal, akipiga picha ya kumbukumbu na baadhi ya kinamama wanachama wa Jumuiya hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimia na baadhi ya watanzania hao ikiwa ni sehemu ya kuwaaga baada ya hotuba yake.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakhia Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa jumuiya hiyo baada ya kuwahutubia.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakhia Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wanachama wa jumuiya.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio New York na vitongoji vyake, Haji Hamis, akizungumza na kutoa utambulisho wa viongozi na wanachama wa Jumuiya hiyo, ambao hadi sasa wamefikia 110.
Baadhi ya Watanzania waishio New York na vitongoji vyake wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed gharib Bilal, alipokuwa akiwahutubia.
Baadhi ya Watanzania waishio New York na vitongoji vyake wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed gharib Bilal, alipokuwa akiwahutubia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal na mkewe, Mama Zakhia Bilal, Balozi Obeni Sefue na Waziri Juma Duni Haji, wakisimama na kuimba wimbo wa maalum baada ya kuwasili kwenye eneo la hafla hiyo.
Bi Fatma (kushoto) na Asha wakipozi kwa picha.
Bi Fatma (kushoto) na Asha wakipozi kwa picha.
Katika hafla hiyo hata viongozi wa Jumuiya hiyo hawakuwa nyuma katika kutekeleza majukumu yao kama kawaida japo ilikuwa ni jumapili, hapa ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Miriam Abu (kushoto) na Mweka hazina msaidizi, Mzee Temba, wakiwa na nyaraka zao ambapo pia walikuwa wakiendelea na zoezi la kusajiri Watanzania wapya waliokuwa wakitaka kujiunga na Jumuiya hiyo.
Jumuiya hiyo ilianza kuwa active zaidi baada ya uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi wa kuiongoza uliofanyika mwezi April mwaka huu na kuwapata viongozi wapya kama Mwenyekiti, Haji Hamis na Makamu wake huyo, Katibu Vicent Mughwai na Katibu msaidizi, Shaban Mseba na Mweka Hazina, Phillip Lwiza na msaidizi wake, Mzee temba na sasa Jumuiya hiyo imejipangia majukumu na malengo mengi ikiambatana na mikakati kabambe ya kuwawezesha kusonga mbele katika kujikwamua kiuchumi na kuweza kusaidiana kimaisha.

No comments:
Post a Comment