Habari za Punde

*EXTRA BONGO KUSHAMBULIA CLUB MASAI ILALA LEO

 Na Michael Maachellah
BENDI mahiri ya muziki wa Dansi nchini Extra Bongo, ‘Wazee wa Kujinafasi’  leo wataporomosha shoo kabambe kwa wakazi wa Ilala Jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Klabu ya Masai.

Akizungumza na mtando huu Meneja wa Bendi hiyo , Muibu Hamisi alisema wakazi wa Ilala watarajie kupata burudani ambayo hawajawahi kuipata kwa kipindi kirefu kutokana na kundi hilo kujinoa vilivyo ili kuweza kutoa burudani ya kina kwa mashabiki wake.

Aliwataka mashabiki wa muziki wa dansi wa maeneo ya Ilala kujitokeza kwa wingi kushuhudiaa mambo mapya na  Style na shoo mpya za bendi hiyo pamoja na rap mpya kutoka kwa rapa mahiri Fergason na sauti murua za waimbaji kama,Rogati Hega Katapiler,Rama Pentagoni, Athanas Motanabe,Bob Kisa,  wakiongozwa na Mkurugenzi wa Bendi hiyo,  Ally Choki.
Aidha alisema kuwa baada ya kukonga nyoyo za Waheshimiwa Wabunge mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita, sasa bendi hiyo Imerejea jijini na kujipanga katika kutoa burudani kwa mashabiki wake.  
Muhibu, alisema kuwa baada ya shoo ya leo kesho Alhamis watakuwa Mzalendo Pub ukumbi wa nyumbani ambapo wakinadada kiingilio ni bure na kwa kinakaka ni Tsh 5000/= na Ijumaa watakuwa Zonghwaa Victoria, Jumamosi Mbagala Zakhem na Jumapili watamalizia ‘Week end’ kwa wakazi wa Mabibo.  

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.