Mashabiki na wapenzi wa timu ya Yanga ya Dar es Salaam, wanaitakia ushindi timu yao inayoshuka dimbani leo jioni kuwakabiri St. George katika mchezo wa nusu fainali utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini. Iwapo Yanga itawagalagaza St. George basi itakuwa ni uso kwa uso na watani wao wa jadi Simba ambao tayari wameshajikatia tiketi ya fainali hizo wakiendelea kusubiri mshindi wa mchezo wa leo. Iwapo timu hizo za Yanga na Simba zitafanikiwa kukutana katika fainali hizo basi itakuwa ni mara ya kwanza baada ya timu hizo zote kuwa na walimu wanaotoka nchi moja Uganda na pia zikiwa na wachezaji nyota waliosajiliwa msimu huu kujiandaa na Ligi Kuu ya Tanzania Bara inayotarajia kuanza hivi karibuni, hivyo itakuwa ni moja jaribio la kuwaona wachezaji wote wageni wakitarajiwa kufanya mambo makubwa katika mchezo huo iwapo watakutana katika fainali hiyo.
Nishati : TANESCO Mmefanya Mageuzi Makubwa katika Huduma ya Umeme kwa
Wananchi - Mhe. Ndejembi
-
Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amesema kuwa Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) limeendelea kufanya mageuzi makubwa katika kuboresha
upatikan...
12 hours ago

No comments:
Post a Comment