Licha ya serikali kugawa vyandarua kwa wananchi kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa malaria lakini baadhi ya wananchi wamekuwa wakitumia vyandarua hivyo kinyume na martumizi kama inavyoonekana moja kati ya chandarua kikitumika kama pazia katika moja ya choo katika kijiji cha Mtandi Kilwa.
Kuelekea sherehe za Uhuru wengine bado hawajajua wala kutambua umuhimu wa sherehe hizo kutokana na kuelemewa na ugumu wa maisha. "Haya ni Makazi ya baadhi ya wananchi wa Kusini ambao kwao bado ni ndoto kuishi katika nyumba iliyoezekwa kwa bati, Katika Kijiji hicho hakuna nyumba hata moja iliyoezekwa kwa bati"
BARABARA YA MINGOYO KIBITI HATARINI KUKATIKA NA MMOMONYOKO
Barabara kuu ya Mingoyo-Kibiti ambayo imetumia mamilioni ya shilingi katika ujenzi wake ikiwa imeanza kuharibika ndani ya miaka 2 tangu kujengwa kwake kufuatia mkandarsi aliyejenga barabara hiyo kujenga chini ya kiwango kama inavyooneka ikiwa imeanza kumeguka kingo zake katika kijiji cha Kiranjeranje Wilayani Kilwa mkoa wa Lindi. Picha Zote na Muhidin Amri, Songea
No comments:
Post a Comment