Habari za Punde

*NAIBU SPIKA ATUNUKIWA TUZO YA CPA LONDON

 Ngao ya Tuzo ya CPA aliyotunukiwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai.

Mwakilishi wa Chama cha Wabunge wanawake wa Jumuiya ya Madola Afrika (CPA) katika Mkutano Mkuu wa 57 wa CPA Dunia Mhe. Beatrice Shelukindo, akipokea tuzo ya CPA kwa niaba ya Naibu Spika Mhe. Job Ndugai,  kutoka kwa Mwenyekiti wa CPA anayemaliza muda wake Mhe. Mohamed Shafie Apda,l kutoka Malaysia ambayo Ndugai, amezawadiwa kwa kuitumikia Kamati tendaji ya CPA kwa muda wa Miaka mitatu.
Mhe. Ndugai amekuwa mjumbe wa Kamati kuu tendaji ya CPA tangu mwaka 2008 ambapo muda wake umekwisha mwaka huu.  Mkutano huo Mkuu wa CPA umemalizika Jana jijini London Uingereza. Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda, akifurahia jambo na Spika wa Bunge la Malawi Mhe. Henry Chimuntu Banda baada ya kumalizika rasmi kwa mkutano wa 57 wa CPA ambao ulifanyika London Uingereza kwa kukutanisha  Maspika, Maseneta na Wabunge zaidi ya 700 kutoka nchi 52 za Jumuiya ya Madola kujadili masuala mbalimbali yahusuyo uendeshaji wa Mabunge katika mabunge wanachama wa Jumuiya hiyo .
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) akiwa katika picha ya Pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Uingerza  Mhe. Nigel Evance (Mb) (Mwenye tai) pamoja na Mwenyekiti Mpya wa CPA Mhe Sir Alan Heselhurst (Mb) mara baada ya kumalizika rasmi kwa mkutano wa 57 wa CPA ambao ulifanyika London Uingereza kwa kukutanisha  Maspika, Maseneta na Wabunge zaidi ya 700 kutoka nchi 52 za Jumuiya ya Madola kujadili maswala mbalimbali yahusuyo uendeshaji wa Mabunge katika mabunge wanachama wa Jumuiya hiyo . Wengine katika picha ni Ujumbe wa Tanzania ulioambatana na Mhe. Spika katika Mkutano huo na Katibu Mkuu wa CP Dkt William Shija ( Nyuma ya Spika) Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge
Naibu Spika wa Bunge la Uingerza  Mhe. Nigel Evance (Mb) (Mwenye tai) pamoja na Mwenyekiti Mpya wa CPA Mhe Sir Alan Heselhurst (Mb) baada ya kumalizika rasmi kwa mkutano wa 57 wa CPA ambao ulifanyika London Uingereza kwa kukutanisha  Maspika, Maseneta na Wabunge zaidi ya 700 kutoka nchi 52 za Jumuiya ya Madola kujadili maswala mbalimbali yahusuyo uendeshaji wa Mabunge katika mabunge wanachama wa Jumuiya hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.