Miss Ilala 2011, Salha Israel, (katikati) akiwa pamoja na warembo wenzake msindi wa pili Alexia William (kushoto) na mshindi watatu Jenifer Kakolaki, baada ya kutangazwa washidi katika shindano lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Viwanja vywa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Warembo hao wamejipatia tiketi ya kushiriki shindano la kitaifa la Vodacom Miss Tanzania 2011.
Ofisa udhamini wa Vodacom Tanzania, Ibrahim Kaude, akimpongeza Miss Ilala 2011, Salha Israel, baada ya kutangazwa mshindi na kujikatia tiketi ya kushiriki katika shindano la kitaifa la Vodacom Miss Tanzania pamoja na wenzake mshindi wa pili na watatu.
Warembo waliofanikiwa kuingia katika nafasi tano bora katika shindano la kumtafuta miss Ilala 2011.
Mrembo, Alexia William, akijibu swali na kuweza kujipatia ushindi wa namba mbili na kuweza kujikatia tiketi ya kushiriki shindano la kitaifa la Vodacom Miss Tanzania 2011.
Mmoja wa washiriki wa Miss Ilala akionyesha kipaji chake cha kuchezea nyoka katika shindano la kumtafuta Miss Ilala 2011.
No comments:
Post a Comment