Habari za Punde

*USIKU WA WAREMBO BOMBA WA KINO, TMK NA ILALA SUNSIRRO

 Baadhi ya warembo wa Kanda za Miss Kinondoni, Ilala na Temeke wakicheza muziki ndani ya Club ya Sun Sirro iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya usiku wa warembo uliondaliwa na Vodacom Tanzania. Kampuni hiyo ndio wadhamini wakuu wa shindano la Vodacom Miss Tanzania mwaka huu.
 Warembo hao wakiendelea kusebeneka, mwenye Kiduku hayaaaa, sebene hayaa ilimradi ni kuchele na furaha.
 Warembo hao wakipita jukwaani wakati wa utambulisho na kumbukumbu......
 Mtaalam wa Masuala ya Habari wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu (Wa pili kushoto) na Ofisa Huduma na Bidhaa wa kampuni hiyo Elihuruma Ngowi (kulia) wakijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Kinondoni, Boy George (katikati) wakati wa hafla hiyo ya usiku wa   warembo wa Kinondoni, Temeke na Ilala. Vodacom Tanzania ndio wadhamini wakuu wa shindano la Vodacom Miss Tanzania mwaka huu.
 Warembo hao wakikumbukia enzi zao kupozi kimiss, hapa ni wakati wakiwa mbele ya kamera.....
 "Eeheee! unakumbuka siku ile ya shindano letu we ulicheza sana wakati wa shindano la kipaji, leo vipi"??, aaah! siku hizi me nimekuwa hata siwezi kucheza tena kama vile......
Hapo, Hapo, Hapo Hapooooo Chachaaaaaaa!

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.