Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo. |
KATIBU Mkuu Kiongozi, Philemn Luhanjo, ametangaza rasmi kumrejesha kazini Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, baada ya kumalizika kwa uchunguzi dhidi yake kuhusu tuhuma zilizotolewa na baadhi ya wabunge Julai 18, mwaka huu ya kwamba alikuwa akitembeza mahela kwa wabunge hao ili waweze kufanikisha na kupitisha bajeti ya Wizara hiyo, ambayo ilishindwa kupitishwa kutokana na mapungufu na kurudishwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, alisema kuwa baada ya Kamati iliyoundwa kufanya uchunguzi wa sakala hilo kutoa ripoti yake Bwana, Jairo, aliyekuwa amepewa likizo iliyokuwa na malipo, ameonekana kutokuwa na hatia na kwamba madai yaliyokuwa yametolewa dhidi yake yalikuwa si ya kweli.
No comments:
Post a Comment