Habari za Punde

*KANALI MUAMMAR GADDAFI HOI WAASI WAUTEKA MJI WA TRIPOLI

Muammar Gaddafi.
 Picha za televisheni zinaonyesha waasi katika wakiwa katika uwanja walioupa jina jipya baada ya kuuteka wa  'Green Square' katika mji mkuu, huku makundi ya watu wenye furaha wakisheherekea kuwasili kwa waasi hao katika uwanja huo.

Imeelezwa kuwa waasi wamemkamata mtoto wa Gaddafi, Saif al-Islam, huku kiongozi mwenyewe akiahidi kuwa ataendelea kupigana.
Mwendesha mashtaka wa mahakama ya uhalifu wa kivita, Luis Moreno Ocampo, amethibitisha kukamatwa kwa mtoto wa Gaddafi, Saif al-Islam, na ambaye alitarajiwa kumrithi kiti cha uirais  sasa amekamatwa.
Mwanawe wa kwanza wa Gaddafi, Mohammed Al Gaddafi, naye amejisalimisha kwa waasi na amewekwa chini ya ulinzi huko ndani ya makaazi moja mjini Tripoli.
Serikali ya Libya imesema takriban wanajeshi elfu 65 watiifu kwa kanali Gaddafi wamebakia mjini Tripoli lakini ni wachache tu walioonekana wakati waasi walipokuwa wakielekea kuuteka mji huo.
Mapigano yameripotiwa katika maeneo mengine ya mji. ambapo waasi wanajaribu kushika udhibiti wa jengo ambalo hutumiwa na waandishi wa habari.
Inaaminika kuwa bado Kanali Gaddafi ana maelfu ya wafuasi waliojihami, japo ripoti zinaashiria kuwa idadi kubwa wamejisalimisha kwa waasi.
Msemaji wa serikali ya Libya , Moussa Ibrahim, amesema takriban watu 1300 wameuwawa mjini humo.
Awali Kanali Gaddafi aliwataka raia kujitokeza na kuukomboa mji wa Tripoli. '' Jitokezeni, jitokezeni niko nanyi. Msirudi nyuma. Tutapigana hadi kuikomboa nchi yetu kuzuia uthibiti. Msiwakubalie wanyakuzi kuiteka nchi yetu, nitapigana pamoja nanyi kama nilivyoahidi'', Alisema Muammar Gaddafi.
Waasi wa Libya wakithibiti mji wa Tripoli.
Usiku wa kuamkia leo wapiganaji waliokuwa wakipambana na vikosi vya Gadaffi, hatimaye wamefanikiwa kuuteka mji wa Tripoli.  

Mamia ya Walibya wanaripotiwa kuingia mitaani kusherehekea ukombozi kutoka kwa utawala wa kidikteta na kikandamizaji, huku baadhi ya watu wakionekana wakichoma moto picha za Gaddafi.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.