Habari za Punde

*NGELEJA SIKIA HII, KINSHASA KUWASHA MISHUMAA


Makundi ya wanaharakati katika Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, yametoa wito kwa wakaazi wa mji mkuu, Kinshasa, kuwasha mishumaa leo usiku, ikiwa ni sehemu ya kufikisha ujumbe wao wa kulalamika juu ya kukatwa kwa umeme.

Ingawa Congo ina maporomoko ya maji yanayoweza kuzalisha umeme kwa wingi, lakini hata hivyo mitambo iliyochakaa na kina cha maji kupungua kwenye mabwawa makuu, kumepunguza umeme kwa kiasi kikubwa hadi kufikia kuathiri biashara, hospitali na shughuli nyengine na hivyo kuyumbisha Uchumi wa nchi.
Kila mmoja kati ya wakaazi milioni 10 wa Kinshasa wameombwa wawashe mishumaa kwa wakati mmoja, katika barabara, nyumba, maduka na roshani.
Wanaharakati wanataraji mishumaa italeta mwangaza katika mji ambao mara nyingi uko gizani.
Aidha wanaharakati hao wametoa ushauri kwa wale wasiokuwa na uwezo wa kununua mishumaa kufanya tendo la kugonga sufuria.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.