Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT BILAL MGENI RASMI FAINALI ZA MASHINDANO YA KUHIFADHI QUR-AN YA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma Hotuba yake  wakati wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur-an, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, leo  na kushirikisha jumla ya wshiriki 14 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakiwa katika ukumbi wa Diamondi Jubilee jijini Dar es Salaam, leo wakifuatilia kwa makini fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur-an.
Mshiriki wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, ambaye alishika nafasi ya kwanza  katika mashindano hayo,  Jahuddin Adam,  kutoka Sudan  akishiriki mashindano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo ambapo mgeni rasmi wa fainali hiyo iliyowashirikisha washiriki 14 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati, alikuwa ni  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Mshiriki kutoka Nigeria, Hashim Thani, akishiriki fainali za mashindano hayo katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam leo.
Mshiriki kutoka KenyaYusuph Mursal, akishiriki fainali za mashindano hayo katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam leo.
Wshiriki kutoka katika nchi za Ethiopia, Tanzania, Sudan, Kenya, Mozambiq, Uganda, Nigeria, Burundi, Afrika ya Kusini, Egypt na Somalia na wakiwa ukumbini hapo wakati wakisubiri utaratibu wa kupanda jukwaani kushiriki shindano hilo katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi , Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakati wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur-an, zilizofanyika leo kwenye ukumbi wa Diamondi Jubilee jijini Dar es Salaam, na kuwashirikisha washiriki 14, kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na baadhi ya Viongozi wa dini ya Kiislamu, wakiwa katika picha ya pamoja na washindi wa kwanza hadi wa tatu wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur-an, baada ya kutangazwa washindi.
 Watangazaji wa Clouds TV wakiwa bize ukumbini hapo kurusha live mashindano hayo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na baadhi ya Viongozi wa dini ya Kiislamu, wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa  fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur-an, baada ya kumalizika kwa mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.