Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige |
Serikali ya Tanzania imemsimamisha kazi, Mkurugenzi wa Wanyamapori, Obed Mbangwa na wasaidizi wake wawili kutokana na kashfa ya kusafirishwa wanyama hai nje ya nchi lililoikumba Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka 2010.
Waziri Maige alisema kuwa, Mbangwa na wenzake, wamesimamishwa kazi kwa malipo kuanzia leo hadi uchunguzi kamili wa suala hilo lililochukua sura mpya na kuwaudhi wabunge na Watanzania wengi kwa ujumla utakapokamilika.
Aidha, amesema hivi sasa inaundwa Tume maalum kwa ajili ya kuchunguza madai ya Mwenyekiti wa Bodi ya Hifadhi ya Ngorongoro, Pius Msekwa, ya kugawa viwanja ndani ya hifadhi hiyo kwa wawekezaji ili wajenge hoteli kinyume cha mamlaka yake.
Maige alisema Tume hiyo itachunguza na kuangalia nini kinafanywa na Bodi na ikigundulika, kuwa tuhuma hizo zinaukweli ndani yake, hatua za kisherika zitachukuliwa dhidi ya mhusika ama wahusika.
No comments:
Post a Comment