Na Juma Nyumayo, Songea
WATU sita wamefariki papo hapo na wengine wawili akiwemo mtoto wamejeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka na kuwaka moto katika kijiji cha Chunya kilichopo wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.
Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Machael Kamuhanda amesema kuwa tukio hilo limetokea juzi (28.8.2011) majira ya saa 12 jioni.
Kamuhanda amebainisha miongoni mwa waliofariki miili yao kuwa imeuungua vibaya huku maiti hizo zikiwa hazitambuliki.
Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo limehusisha Gari lenye namba za usajili T 270 BDG Landrover likiwa linaendeshwa na Dereva Stevin Ngoko (32) kupinduka na kuwaka moto na kusababisha vifo vya watu sita papo hapo katika kiji cha Chunya barabara iendayo Mbambabay toka Mbinga.
Kamanda Kamuhanda amewataja waliojeruhiwa katika ajari hiyo kuwa ni Jeremia Masalo (38) mkazi wa nchi jirani ya Msumbiji na Anna Godrfei (3) mkazi wa Mbambabay ambao wote wamelazwa katika Hospitali ya Serikali ya Wilaya ya Mbinga kwa matibabu.
Alisema kuwa watu waliokufa majina yao hayajaweza kufahamika kutokana na maiti hizo kutotambulika kwa kuwa zimeungua vibaya na zote zimepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya hiyo.
Kamanda Kamuhanda alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi ambao ulimsababishia dereva wa gari hilo kushindwa kumudu usukani na kwamba jeshi lake linaendesha msako wa kumtafuta dereva wa gari hilo Bw. Ngoko ambaye alitoroka mara tu baada ya kutokea ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment