Wanafunzi wa Madrasatul Shamsia ya Mafia, wakipokeamsaada wa katoni ya sabuni kutoka kwa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, Mwamvita Makamba.
Vodacom kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa 'Vodacom Foundation' ilitoa sadaka ya vyakula kwa ajili ya futari kwa wanafunzi zaidi ya 300 wa madrasa mbalimbali za wilayani humo pamoja na kuwafuturisha mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule (katikati) na Imam Mkuu wa Msikiti mkuu wa Mafia, Ally Mwabaku.
Wanafunzi wa Al-Madrasatul Hairislamia ya Mafia wakibeba kiloba cha mchele kwa furaha baada ya kukabidhiwa msaada wa sadaka ya futari kwa ajili ya mfungo wa Ramadhani. Vodacom kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation ilikabidhi sadaka kwa wanafunzi zaidi ya mia tatu wa madrasa mbalimbali za kisiwani Mafia yenye thamani ya zadi ya shilingi milioni 9 ikiwa ni sehemu ya kampeni ya 'Share and Care' ambapo kwa mwezi wa Ramadhan hulenga kufuturisha waislamu na kutoa sadaka ya futari kwa watoto hususan yatima na wajane.
. Mkuu wa mfuko wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule, akimhudumia mmoja ya waumini wa dini ya Kiislamu wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na mfuko huo katika msikiti mkuu wa wilaya Qadiriya na kuhudhuriwa na waislamu mbalimbali wakiwemo watoto zaidi ya 300 kutoka madrasa zilzopo wilayani humo.

Meneja Mawasiliano wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, Salum Mwalim, akimhudumia futari shekhe Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Sheikh Yusuf Selemani, wakati wa hafla ya kufuturisha wasilamu na watoto wa madrasa kisiwani Mafia.
No comments:
Post a Comment