Kuelekea miaka 50 ya Uhuru bado wapo wasioendana na maadhimisho ya shere hizo, tena wengine ni ndani ya Jiji kubwa kama hili la Bongo ambao wamekuwa na matatizo lukuki kila kukicha kuhusu Umeme, Maji na huduma nyingine muhimu za kijamii, Je ni lini wabongo yaani Watanzania wa mijini na Vijijini, wataishi bila maisha ya mashaka? Kama walivyokuwa Walybya kila kitu bure na bado wanahitaji mageuzi. Waswahili husema kila amuombaye Mungu hupewa lakini mbona wabongo hawapewi? Na hata Wananchi wa Lybya, ipo siku watalia na kusaga meno kwa wanachokiomba kwa sasa baada ya kuona uongozi wa miaka 40 ya Kanali Gaddafi, wa kupewa huduma zote muhimu bure hauwafai "ipo siku watamkumbuka Gaddafi", na hii sidhani kama imewahi kutokea hata katika nchi Taifa kubwa na yenye uwezo iliyoweza kuwahudumia wananchi wake kwa kuwapa huduma muhimu bure na wengine kuhozwa wake na serikali, Elimu, Nyumba na mengineyo, Hii aliiweza Gaddafi pekee
Hili ni Tangazo linalowahusu wakazi wa Kijiji kimoja katika Mkoa wa Iringa, ambao kwao Nyama imekuwa ni kitendawili, na kama hivyo ndivyo kwa kitoweo kama nyama imekuwa ni kitendawili kama hivi, vipi kuhusu Umeme na maji si ndi mpaka Yesu arudi??
No comments:
Post a Comment