Habari za Punde

*YANGA, SIMBA ZABANIWA UWANJA WA TAIFA, MUMBARA 'BADO YUPO YUPO KWANZA' KUICHEZEA TOTO AFRICA


Boniface Wambura,

Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
AKIZUNGUMZA na waandishi wa habari leo mchana Ofisa habari wa Shirikisho la Mpira            wa miguu Tanzania, Boniface wambura, alisema kuwa baada ya Serikali kuufunga  Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa ajili ya marekebisho, timu za Yanga na Simba  ambazo awali zilikuwa zimeruhusiwa kutumia uwanja huo kwa ajili ya mechi za Ligi  Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, zimelazimika kutafuta viwanja vipya. 

Ambapo timu ya Simba imehamia Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wakati Yanga iko Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro.

RATIBA YA LIGI KUU MZUNGUKO WA KWANZA
"Licha ya timu hizo kupata viwanja vipya ratiba itabaki kama ilivyotolewa awali, ambapo mechi za Simba zilizokuwa zichezwe Uwanja wa Taifa sasa zitachezwa Mkwakwani wakati za Yanga zitachezwa uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, 

Kutokana na mabadiliko hayo ratiba inasomeka kuwa Septemba 7 mwaka huu Coastal Union v Moro United (Uwanja wa Mkwakwani) na pia Simba v Villa Squad (Uwanja wa Mkwakwani). 

Mechi ya Simba v Villa Squad imesogezwa mbele kwa siku moja ambapo sasa itachezwa Septemba 8 mwaka huu kwenye uwanja huo huo" alisema Wambura

MCHEZAJI CASTORY MUMBARA
Aidha TFF imeshindwa kumpa leseni Castory Mumbara, ambaye ameombewa usajili katika timu ya Toto Africans kutokana na kutokuwa na Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) ambayo inatakiwa kutolewa kupitia mfumo wa mtandao wa Transfer Matching System (TMS).

"Ikumbukwe kuwa Mumbara, alikuwa akichezea timu ya Himalayan Sharpa ya Nepal, ambapo alikwenda huko baada ya TFF kumpatia ITC, 

Hivyo ili aichezee Toto Africans, klabu hiyo ilipaswa kumuombea hati hiyo kupitia mtandao wa TMS baada ya kufanya mawasiliano na Himalayan Sharpa.

Muda wa usajili ulimalizika Julai 31 mwaka huu, hivyo Toto Africans kwa sasa haiwezi kumtumia mchezaji huyo, badala yake inatakiwa kusubiri dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa tena Novemba mwaka huu. 

TFF iliendesha mafunzo ya kutumia mfumo wa TMS kwa watendaji wote wa klabu za Ligi Kuu ikiwemo Toto Africans".

MECHI YA STARS v ALGERIA
Mechi hiyo namba 103 ya mchujo wa kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani, Equatorial Guinea na Gabon itachezwa nchini Septemba 3 mwaka huu.

"Lakini bado tunasubiri majibu ya ombi letu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo la kuturuhusu kutumia Uwanja wa Taifa kwa ajili ya mechi hiyo", alisema wambura

ALL AFRICA GAME
Mwamuzi msaidizi John Kanyenye wa Tanzania ni miongoni mwa waamuzi 32 (waamuzi wa kati na wasaidizi) walioteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuchezesha michezo ya All Africa Games itakayofanyika Maputo, Msumbiji kuanzia Septemba 3-18 mwaka huu. 

Aliwataja waamuzi hao kuwa ni Kati ya hao, 16 ni wanaume na 16 ni wanawake.

"Kanyenye ni mmoja kati ya waamuzi watatu kutoka  ukanda wa CECAFA- Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati walioteuliwa kuchezesha michezo hiyo, 

Wengine ni mwamuzi wa kati wa kike kutoka Uganda, Nabikko Semambo na mwamuzi msaidizi wa kike kutoka Ethiopia, Trhas Gebreyohanis" alisema Wambura
Boniface Wambura 
Ofisa Habari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)




No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.