Habari za Punde

*WAJEDA WAHARIBU MALI NA MAKAZI YA WANAKIJIJI WAPATAO 200 KIMBIJI


*Uvamizi wa wanajeshi dhidi ya wanakijiji Kimbiji, Polisi kigamboni wageuka 'MABUBU'
*Wagoma kupokea malalamiko ya wanakijiji, Nani wa  kumfunga Simba kengele?

Uvamizi na uharibifu wa mali na mashamba ya raia uliofanyika Agosti 16, mwaka huu siku ya jumatano mida ya saa nne asubuhi katika kijiji cha Kimbiji, nje kidogo ya Jiji la Dar, wananchi wamebaki na mashaka ya maisha yao baada ya makazi na mazao yao kuharibiwa na kuamua kumuachia 'MUNGU" 

Uharibifu huo umedaiwa kufanywa na wanajeshi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ambao walivamia kijiji hicho na kuvunja makazi ya raia kinyume cha sheria. 

Hata hivyo baadhi ya wanakijiji waliamua kupeleka taarifa hizo katika vituo vya polisi vya Kigamboni na mji Mwema, lakini cha ajabu walipofika katika vituo hivyo, wahusika wa vituo vya Polisi waligoma na kukataa kata kata kupokea malalamiko ya wanachi hao, walioharibiwa mali zao.

Katika Sakata hilo la wanajeshi (JWTZ) kuvamia makazi ya raia na kuharibu mali za raia
bado lina utata  ambao haijulikani ukweli wa jambo hilo upo wapi? SASA katika tukio hili Nani ni Nani na Nani wa Kumfunga simba Kengele?, walihoji baadhi ya wanakijiji baada ya kukosa pa kupeleka malalamiko yao.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.