Habari za Punde

*WANAFUNZI MWAKA WA KWANZA CHUO CHA RUCO WADAI PESA ZA FIELD

Mkuu wa Chuo cha Ruaha (Ruco)

UJUMBE KUTOKA KWA WANACHUO WA RUCO IRINGA
"SISI ni wanachuo wa mwaka wa kwanza BAED chuo cha Ruaha Iringa (Ruco), tatizo letu kubwa ni kucheleweshewa pesa zetu kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo(Field) na tatizo hilo hasa ni kwa wale tunaotumia bank ya NMB, imekuwa ni kawaida kwa chuo chetu kutucheleweshea pesa hasa tunapokuwa katika likizo. 

Ni mwezi sasa toka tumeanza field lakini kila siku ni kuzungushwa tu mara bodi ya mikopo haijatoa cheque, mara cheque tushapeleka bank ya nmb mara cheque iko kwa uhasibu sasa kaka ukiwa kama wewe ni mkombozi wetu tunaomba ufuatilie matatizo yetu haya na ikibidi uweke hata kwenye blog yako ili waweze kutuharakishia maana bado week mbili tuu tumalize, hebu fikiria kaka hawa daa zetu wanaishije kama sio kujiuza? 

Tunatambua kuwa serikali yetu ni sikivu hivyo tunaomba waziri wa elimu kusikia kilio chetu na kufika hapa chuoni ili kusikia kilio chetu kwani tunaishi katika mazingira magumu zaidi hapa chuoni.
 

Tunakuomba sana tena sana utusaidie katika hili maana tunategemea sana mtandao huu kama sauti yetu wanyonge katika kudai haki zetu na kujua mambo mbali mbali katika taifa na nje ya Taifa na tatizo lingine linalotupelekea tuone kuwa hili ni
 dili ni kuwa hamna ufuatiliaji wowote unaotoka Chuo na pia hata serikali ya wanafunzi ya chuo imekaaa kimya kabisa laiti ikijua kuwa hayo ni moja ya majukumu yao. 

Ombi letu kwa uongozi wa mtandao huu na vyombo vingine vya habari zitakavyopata habari hii kupitia mtandao huu kutusaidie katika hili ili tuweze kupata hizo pesa week hii
 vinginevyo hatutaona shida kuandamana hadi kwa mkuu wa mkoa wa Iringa kudai haki zetu . 

MUNGU AKUBARIKI SANA KATIKA KAZI ZAKO"
. 

Ni SISI WANACHUO RUCO (majina yamehifadhiwa)

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.