Habari zilizoufikia mtandao huu hivi punde zinaeleza kuwa Meli ya abiria ya Spice iliyokuwa ikitoka Unguja kuelekea Pemba, imezama usiku wa kuamkia leo eneo la Nungwi na kuuwa idadi yote ya watu waliokuwamo wanaokadiliwa kuwa 1,500.
Aidha imeelezwa kuwa meli hiyo iliondoka katika Bandari ya Unguja jana jioni ambapo ilitarajia kutia Nanga katika Bandari ya Pemba leo asubuhi.
Imeelezwa kuwa Meli hilo ilianza kuyumba baada ya kufika maeneo hayo ya Nungwi, eneo ambalo huwa na misuko suko na mawimbi makubwa na kina kirefu cha maji.
Mtandao huu unawapa pole wale wote waliokutwa na msiba huu mkubwa, na pia tutaendelea kuwajuza kila kitakachoendelea juu ya tukio hili.
No comments:
Post a Comment