Baadhi ya wageni waalikwa kutoka Balozi mbalimbali nchini, Taasisi za Kiserikali na zisizo za kiserikali wakifuatilia picha zilizokuwa zikionyeshwa katika maonyesho hayo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mtandao wa Maendeleo kutoka Taasisi ya Aga Khan, Navroz Lakhani, ambao ni miongoni mwa wadhamini wa maonyesho hayo akizungumza machache katika hafla hiyo ya ufungaji wa maonyesho hayo.
miongoni mwa wadau mbalimbali kutoka sehemu na Idara Tofauti za ndani na nje ya nchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea katika hafla hiyo ya maonyesho ya picha yanayoelezea ushirikiano wa nchi ya Brazil na zile za kiarabu katika nyanja mbalimbali.
Baadhi ya wadau kutoka Idara Tofauti za ndani na nje ya nchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea katika hafla hiyo ya maonyesho ya picha yanayoelezea ushirikiano wa nchi ya Brazil na zile za kiarabu katika nyanja mbalimbali.
Ofisa Ubalozi, Lucy Mwambungu (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na msanii wa siku nyingi wa michezo ya Kuigiza maarufu kama Sinta pamoja na Makamu wa Balozi wa Brazil nchini, Ronaldo Vieira.
No comments:
Post a Comment