Habari za Punde

*MAPRO WA YANGA WAANZA KAZI LIGI KUU

Kikosi cha timu ya Yanga, kilichoshuka dimbani katika Uwanja wa Chamanzi Mbagala jijini Dar es Salaam jana kumenyana na Villa Squad na kuibuka na ushindi wa mabao 3-2, huku mabao hayo yakiwekwa kimiani na wachezaji wa kulipwa wa timu hiyo.

Magoli hayo yalifungwa na Keneth Asamoh, Hamis Kiiza aliyeingia kipindi cha pili na Haruna Niyonzima.

Kwa ushindi huo sasa Yanga imefikisha jumla ya Point 9 ikishika nafasi ya sita, huku nafasi ya kwanza ikiendelea kubaki kwa Simba ambao nao walibanwa mbavu na Toto Africa ya Mwanza baada ya kutoka sare ya mabao 3-3 katika mchezo wao uliopigwa katika Uwanja wa CCM Kirumba.

 Nafasi ya pili inashikwa na Azam FC, ambao nao waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo wao uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga jana.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.