Habari za Punde

*MASHINDANO YA SHIMIWI YAZINDULIWA RASMI JIJI DAR

 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejiment Utumishi wa Umma, George Yambesi, akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi mbalimbali za Kiserikali waliohudhuria katika mazoezi ya pamoja kwenye Viwanja vya TTC Chang'ombe jana, wakati wa mazoezi hayo yaliyokuwa rasmi kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa mashindano ya Shimiwi yanayotarajia kuanza kutimua vumbi Novemba 5 hadi 18 Mkoani Tanga mwaka huu. 
Baadhi ya wafanyakazi, wakiwa katika mazoezi ya pamoja wakati wa uzinduzi huo uliofanyika jana katika Viwanja vya TCC Chang'ombe.

Hawa pia ni baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Madini, wakiwa bize katika mazoezi hayo.
Wengine walikuwa hoi kiasi kwamba hata mazoezi ya kunyoosha kiuno tu walishindwa kumudu.
Hawa ni baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, wakiwa katika mazoezi hayo.
Wakati wengine wakiwa bize na mazoezi wengine walikuwa bize na mawasiliano ya simu.
Katibu Mkuu, George Yambesi, akijumuika na wafanyakazi katika mazoezi hayo.
Ulifika wakati wa mchezo wa Soka, ambapo zilianza timu za PSPF na Mifugo.
Mchezo wa Soka unaendelea.
Pia ulifika muda wa mchezo wa kuvuta kamba, ambapo zilianza timu za Hazina na Mambo ya Nje, hawa walitoka ngoma droo.

Mchezo wa kuvuta Kamba baina ya Hazina na Mambo ya Nje ngoma ilikuwa Droo.
Mchezo wa kuvuta Kamba unaendelea, upinzani ulikuwa ni mkubwa kamba haisogei hata nukta moja.

Jamaa hawa walikaniana ile mbaya hapa kila mmoja akivuta kamba huku akiwa kakunja uso.
Upinzania wa kamba ukiendelea...
Mchezo wa Netiboli zilianza timu za Elimu na Ulinzi.
Mchezo wa Netibol unaendelea..
Mchuano wa Netiboli unaendelea.
Ni timu za Elimu na Ulinzi zkiendelea kuchuana vikali.
Lilikuwa ni goli la kwanza kufungwa katika mchezo huo.
Ni kama anasema "Hakipiti kitu hapa"
Hatimaye ulianza mchezo wa kuvuta kamba baina ya timu ya Hazina na Mambo ya Ndani, ambao pia nao walitoka sare kwa kutoshana nguvu kama ilivyokuwa kwa timu zao za wanaume ambao nao pia walitoka sare.
Kiukweli ilikuwa ni vuta nikuvute katika mchezo huo baina ya Hazina na Mambo ya Ndani.
Hawa nao walikunjiana sura utazani ni maadui wa kweli kumbe ni mashosti ile mbaya na hasa wanapokutana katika Menu pale Hazina mida ya mchana.
Hapa havutwimtu hapa......
Oya huko nyuma ongezeni nguvu naona wananielemea huku.....
"Jamani eeh! msilegee huko nyuma huyu wao aliye mbele ana nguvu ka faru"......
Hawa pia walikuwa ni miongoni mwa wadau waliohudhuria uzinduzi huo...
Katika uzinduzi huo pia Bendi ya Msondo iliweza kutoa burudani mwanzo mwisho na kuwapagawisha wafanyakazi hao.
Baadhi ya wafanyakazi hao wakiselebuka na sebene la Msondo........
Wengine walikuwa wakisebeneka na miondoko hiyo huku wakiwa na vilaji vya mkononi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.