| | |
Pambano la mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Algeria (Desert Warriors) limeingiza sh.148,220,000. Mechi hiyo ilichezwa Septemba 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mashabiki waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo ni 29,892. Viti vya kijani ambavyo kiingilio kilikuwa sh. 3,000 ikiwa viti hivyo ndivyo vilivyowavutia zaidi mashabiki wengi ambapo 17,650 ikiwa ni zaidi ya nusu ya mashabiki wote walionunua tiketi kwa ajili ya viti hivyo. VIP A ndipo kulikokuwa na kiingilio cha juu cha sh. 30,000, jumla ya mashabiki 394 walinunua tiketi kwa ajili ya eneo hilo. Viti vya bluu kiingilio kilikuwa sh. 5,000, mashabiki walionunua tiketi walikuwa ni 8,166. Viingilio vingine katika pambano hilo vilikuwa sh. 7,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 VIP C na sh. 20,000 VIP B. Boniface Wambura Ofisa Habari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) | |
| | |
| | |
JUWATA, UTPC WAKUBALIANA KUIMARISHA USHIRIKIANO KULINDA UHURU WA VYOMBO VYA
HABARI NCHINI
-
JUKWAA Huru la Wahariri Tanzania (JUWATA) na Umoja wa Klabu za Waandishi wa
Habari Tanzania (UTPC) wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika kulinda
uh...
2 hours ago

No comments:
Post a Comment