Habari za Punde

*NDEGE YAANGUKA UYOLE MBEYA ABIRIA WOTE WANUSURIKA

Ndege yenye namba 9J-BIO SESINA 206, ikiwa imepata ajali katika eneo la Nanenane Uyole Mokani Mbeya leo asubuhi majira ya saa tatu. Katika ajali hiyo ya ndege iliyokuwa imebeba abiria wanne hakuna aliyepoteza maisha.

Akizungumza na Mtandao huu kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Mbeya, Anaclet Malimbisa, alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo hakikuweza kufahamika mapema akidai kuwa bado uchunguzi wa ajali hiyo uanendelea.

Aidha aliwataja abiria waliokuwamo katika ndege hiyo kuwa ni,  Jver Waak miaka (49) ambaye ni Rubani wa ndege hiyo, Raia wa Afrika ya Kusini, Ofisa Utwala wa Mashamba ya Kapunga Wilaya ya Marali,Christina Mmasi (30)  Balozi Mohammed Ramia (64) mkazi wa jijini Dar es Salaam na Sunny Tayir (50)  wotw wakiwa ni wafanyakazi wa Kampuni ya Export Trading Co. 
 Ndege hiyo ikiwa eneo la tukio ikiwa imeharibika baada ya ajali hiyo.
 Ndege hiyo ikiwa imechimba chini na kupinda mapanga boy yake.
Baadhi ya watu waliofika eneo hilo na kutoa msaada kwa abiria waliokuwamo katika ndege hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.