Habari za Punde

*RAIS JAKAYA KIKWETE AWAAPISHA WAKUU WA MIKOA IKULU DAR LEO

 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa walioteuliwa kushika nyadhfa hizo baada ya kuwaapisha katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam leo, asubuhi.
 Rais Jakaya, akimwapisha Mwantum Bakari Mahiza, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo asubuhi katika Viwanja vya Ikulu Dar. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo.

 Rais Jakaya, akimwapisha na kumkabidhi nyaraka za serikali, Joel Nkya Bendera, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Waziri mkuu, Mizengo Pinda, wakati wakiwa katika hafla hiyo ya kuapishwa wakuu wa mikoa leo.
Rais Jakaya, akimwapisha Saidi Meck Sadik, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Rais Jakaya, akimwapisha Fatuma Abubakar Mwassa, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
Rais Jakaya, akimwapisha Magesa Stanslaus Mulongo, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na mtoto Abubakar Mrisho Yasin, akiwa na Mkuu wa Mkoa mpya wa Mkoa wa Chiku Abdallah Sumbugallawa, aliyeapishwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Tanga.

Makamu wa Rais Dkt Bilal, akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantum Mahiza.

Rais Jakaya, akimwapisha Abbas Hussein Kandoro, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Rais jakaya, akimwpisha, Christine Gabriel Ishengoma, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
Rais Jakaya, akimwapisha, Saidi Thabiti Mwambungu, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Rais Jakaya, akimwapisha, Chiku Abdallah Sumbugallawa, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Rais Jakaya, akimwapisha, Leonidas Tutubert Gama, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Rais Jakaya, akimwapisha, Fabian Inyasi Massawe, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.


"Nadhani tumemaliza kazi sasa" Rais jakaya Kikwete, Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiteta jambo baada ya kuwaapisha wakuu wa mikoa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.