Baadhi ya wasanii wa Kundi jipya la Muziki wa Taarab, la Tanzania Moto modern Taarab (T-Moto), wakiwa katika Studio za Makunde Production Kinondoni jijini Dar es Salaam jana, wakati wakirekodi nyimbo zao mpya zitakazokamilisha albam yao ya kwanza ya Aliyeniumba Hajanikosea.
kundi hilo limeingia Studio za Bakunde Production zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam jana kuanza kurekodi nyimbo zake mpya zilizokamilika ili kukamilikamisha albam.
Wasanii wa Kundi jipya la Muziki wa Taarab, la Tanzania Moto modern Taarab (T-Moto), Mosi Suleiman (kushoto) na Hassan Ally, wakiwa katika Studio za Makunde Production Kinondoni jijini Dar es Salaam jana.
Msanii chipukizi katika miondoko ya Taarab, aliyeibukia katika michuano ya BSS, Mrisho Rajab, aliyejiunga na kundi jipya la Taarab la Tanzania Moto Modern Taarab (T-Moto) akiimba kwa hisia wakati akirekodi kibao chake cha Mchimba Kaburi Sasa Zamu yake Imefika, katika Studio za Bakunde Production zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam jana. Wimbo huo ni miongoni mwa nyimbo zinazokamilisha albam yao ya kwanza ya Aliyeniumba Hajanikosea.
KUNDI jipya la Taarab la Tanzania Modern Taarab (T-Moto) linalotarajia kuzinduliwa Oktoba 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam, limezindua mavazi yake rasmi kwa ajili ya kuwazawadia mashabiki wake siku ya uzinduzi.Akizungumza na Mtandao wa Sufianimafoto Blogspot, Mkurugenzi wa Kundi hilo, Amini Salmini, alisema kuwa wameamua kuandaa Tisheti kwa ajili ya wanaume na Vitop vya Kidada, zenye Nembo ya kundi hilo kwa ajili ya mashabiki wa kundi hilo, watakaojitokeza kushudia uzinduzi wao.
Aidha Amini alisema kuwa Ujio wa kundi hilo utakuwa ni tofauti na makundi mengine yaliyopita kutokana na kujiandaa vilivyo na kulifanya kundi hilo kuwa ni la kipekee katika utendaji kazi na kujali maslahi ya kila msanii wa kundi hilo.
“Kwanza kabisa kundi langu nimeangalia zaidi maslahi ya wasanii na kufanya utafiti ni vitu gani wanapendelea zaidi wasanii ili kuweza kufanya kazi kwa bidii na kujituma zaidi, nikaona la kwanza ni maslahi ambayo ndiyo kitu cha kwanza kufanyia kazi na kujipanga zaidi,
Na pia ili kumfanya msanii aweze kuinjoi na kuipenda kazi yake ni lazima awe na mazingira mazuri ya kufanyia kazi ikiwa ni pamoja na vyombo vizuri, ambalo pia nimelipa kipaumbele kwa kuanzisha kundi nikiwa tayari nina vyombo vilivyokamilika na kuongeza ufanisi zaidi kwa kuongeza Gitaa la tatu la rythim jambo ambalo makundi mengine hayajafanya hivyo” alisema Amini
Alisema kuwa ameweka magitaa matatu katika kundi hilo ili kuweza kuongeza radha ya muziki na kuleta uotafauti baina ya nyimbo za kundi hilo na nyimbo za makundi mengine.
Wakati huohuo kundi hilo limeingia Studio za Bakunde Production zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam jana kuanza kurekodi nyimbo zake mpya zilizokamilika ili kukamilikamisha albam.
Mkurugenzi wa kundi hilo, Amini Salmini akiwa ametinga Pamba yenye Nembo ya Kundi hilo. Hivi ndivyo ilivyo Pamba hiyo kwa nyumba Kama inavyosomeka, 'MCHIMBA KABURI SASA ZAMU YAKE...........'
Baadhi ya mashabiki wa kundi hilo waliobahatika kuwa wa kwanza kupata Pamba hizo, waking'ara na kushaini na pamba hizo.
No comments:
Post a Comment