Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TAA) Suleiman Suleiman (kushoto) na Mhandisi Mwandamizi wa Kampuni ya SINOHYDRO CORPORATION LTD, Tawi la Afika Mashariki, Qin Chao, wakitiliana saini mikataba ya ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Kigoma, wakati wa hafla fupi ya kutiliana saini iliyofanyika jijini Dar es salaam leo, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania katika sekta ya Uchukuzi, Sherehe hiyo pia imehudhuriwa na Uongozi wa Wizara ya Uchukuzi. Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TAA) Suleiman Suleiman akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo baada ya kusaini mikataba ya ukarabati wa viwanja vya ndege vya Bukoba, Tabora na Kigoma ikiwa ni sehemu ya maadhiisho ya sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania katika sekta ya Uchukuzi.
Baadhi ya maofisa wa Wizara ya Uchukuzi waliohudhulia hafla hiyo leo.
Picha ya pamoja baada ya hafla hiyo
No comments:
Post a Comment