Habari za Punde

*URBAN PULSE 'ASHINE' NDANI YA SPORAH SHOW!!

Urban Pulse akiwa na Mish na Sporah, wakati wa kipindi maalum cha Sporah Show.
Kwa mara nyingine tena Frank toka Urban pulse na msaniii makini, Fyah Sister, wakiwa ndani ya studio za Televisheni zinazotengeneza kipindi maarufu cha Sporah Show.

Kipindi hiki maarufu kinachoendeshwa na Dada yetu Sporah nchini Uingereza,  kinapatiakana katika Sky TV chaneli 184. Frank na Fyah Sister walialikwa kwenye exclusive interview na Dada Sporah kuzungumzia hali ya promotion ya nyimbo na mixtape ya fyah Sister iliyopo mtaani hivi sasa. 

Vilevile walizungumzia hali ya uhusiano wa ma promoter na wasanii pamoja na changamoto wanazokumbana nazo wasanii.

Album ya Fyah Sister ambayo imetengenezwa katoka studio za urban pulse, ni moja ya albamu zinazokuja juu kwa sasa hasa katika kundi la wasanii wa kike, kwani England kuna wasanii wachache sana wazuri wa kike. 

Pia kipindi hicho kiliongelea hatua na mafanikio ambayo urban pulse wameyapata mpaka sasa kwenye masuala ya mbalimbali. 

Unaweza kudownload au kusikiliza mixtape ya Mish inayoitwa 'Fire Brigade' kupitia link hii hapa chini.


Mish ni msanii mkali wa kike anaekuja juu hapa UK, amefanya maonyesho mengi ikiwepo Notting Hill Carnival, Derby, Centre Hall Westminister jijini london n.k. Pia amechaguliwa kuingia katika mchakato wa kumtafuta best MC katika shindano linaloitwa OPEN MIC litakalofanyika mwezi wa kumi na fainali zake kufanyika katika O2 Arena London.

Spora show imekuwepeo mstari wa mbele katika kusaidia, kuwahamisha wafanyabiashara na wanaharakati wa Kiafrika hapa UK. Vilevile ni kipindi kinachopigania na kuangaza mapambano kuhusu masuala yanayozikabili jamii za kiafrika zilizopo UK, kama vile, domestic violence,child abuse,rape, teenage pregnancy na masuala mengine yanayoathiri jamii zetu.

Kipindi Hiki kitakuwa hewani kupitia Ben TV sky channel 184. Kwa maelezo zaidi tembelea Sporah Show Blog. http://thesporahshow.blogspot.com/
Frank akijadiliana na Mish wakati wa kipindi cha chemsha Bongo.
Picha ya pamoja baada ya show.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.