Habari za Punde

*TBL YACHANGIA HARAMBEE YA MAABARA,GARI ST. MARY'S MOSHI

Meneja wa Shule ya Sekondari ya St. Marry  Goretti, Mtawa Fina Mushi na Mkuu wa shule hiyo Mtawa Lucretia Njau wakimkabidhi zawadi ya kikombe Waziri Mkuu mstaafu,ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Cleopa Msuya (kulia) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 10 ya kidato cha nne yaliyofanyika juzi katika shule hiyo, iliyopo Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro. TBL ilichangia sh. mil. 10 katika harambee ya  kununulia vifaa vya maabara na gari la shule.
Waziri Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya (kushoto) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), akipatiwa zawadi ya picha na wanakamati ya mahafali ya kumi ya Shule ya Sekondari ya St. Mary Goretti ya mjini Moshi juzi,kwa kutambua mchango wake wa maendeleo katika Taifa. Katika mahafali hayo ambayo Msuya alikuwa mgeni rasmi, TBL, ilitoa msaada wa sh. milioni 10 za kusaidia kununua vifaa vya maabara na gari la shule hiyo.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Mkoa wa Kilimanjaro, Leiya Hermenegild (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya sh.mil.10, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya St. Mary Goretti ya mjini Moshi, Mtawa Lucretia Njau. 
Fedha hiyo ilitolewa na TBL kuchangia fedha za kusaidia kunua vifaa vya maabara na gari la shule hiyo. 
Hafla hiyo ilifanyika juzi wakati wa mahafali ya shule hiyo, ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya ambaye pia nia Mwenyekiti wa Bodi ya TBL.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.