Rais Jakaya Kikwete, akifurahia jambo na kukumbatiana na Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba.
Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa na Dr. Wilbrod Slaa, Katibu Mkuu wa CHADEMA.
Wanasiasa wetu wanapokua katika harakati za kuomba kura kwa wananchi kwa nyakati tofauti na kila mmoja wao akimnanga mwenzake kwa hili na lile na kuonyesha kana kwamba wao ni watu walo na utofauti mkubwa, kila mmoja akiwavutia wananchi kuwa upande wake.
Kumbe hii ni tofauti kwa viongozi wetu hawa wao ni marafiki wakubwa na wanaoelewana kuliko hata sisi wananchi tunaogombana wenyewe kwa weneyewe eti kwa sababu ya kiongozi wa chama tunachokipenda.
Tuache haya nasi tuwe kama viongozi wetu kwani wao ni kama wachezaji wa Yanga na Simba upinzani na kusemana vibaya unakuwa ni wakati tu wakiwa katika majukwaa lakini pembeni wao ni washkaji kwisha kazi, tuige mfano huu tusiuane ovyo na kuumizana na kama ilivyo sasa huko Iginga ambako wananchi kwa sasa wao kwa wao wanatofautiana eti kutokana na utofauti wa itikadi zao za vyama vya siasa.
No comments:
Post a Comment