KATIBU wa sekretarieti ya Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania (Hay- Atul Ulamaa) Sheikh Sherally Huseein (kulia) akitoa tamko kwa waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana kuhusu wafuasi wa Chama cha CHADEMA kukaidi kuomba radhi kwa umma wa Kiislamu kufuatia tukio la udhalilishaji kwa kumvua Hijjab Mkuu wa Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Mama Fatma Kimario lililotpkea septemba 15 mwaka huu. Katikati ni Naibu Mwenyekiti wa Umoja huo, Sheikh Abdallah Bawazir na kushoto ni Sheikh Manzi Said Manzi wa taasisi ya MWINYI MKUU. Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO)
Baadhi ya viongozi wa dini ya Kiislam na Masheikh walioandamana na Viongozi wakuu walipofika kutoa tamko.
Naibu Katibu Mkuu wa sekretarieti ya Hay- Atul Ulamaa Tanzania sheikh Mohammad Issa (kulia) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam wakati umoja huo ulipotoa tamko lao la pamoja kuhusu kitendo cha Chama cha CHADEMA kutoomba radhi kwa waislamu kufuatia kitendo cha udhalilishaji wa kumvua hijjab Mkuu wa Wilaya ya Igiunga, mkoani Tabora, Mama Fatma Kimario. Kushoto kwake ni Katibu wa sekretarieti ya Hay- Atul Ulamaa Sheikh Sherally Hussein.
No comments:
Post a Comment