Habari za Punde

*TEVEZ KITANZINI NA ADHABU YA KULIMWA MSHAHARA, MAN CITY

Tevez

Carlos Tevez
Mshambuliaji wa Manchester City Carlos Tevez amepewa adhabu ya kukatwa mshahara kwa wiki nne, ambapo adhabu hiyo imeambatana na onyo la maandishi baada ya kukutwa na hatia ya kukiuka mkataba wake aliosaini wakati akijiunga na timu hiyo akitokea Man U.
Mchezaji huyo kutoka Argentina amepewa pia adhabu ya kutocheza soka kwa wiki mbili, lakini adhabu hiyo tayari amekwisha itumikia, ambapo pia hakuonekana katika kikkosi kilichoiangamiza Man U kwa mabao 6-1 mwishoni mwa wiki iliyopita.
City imemkuta na hatia Tevez ya makosa matano, ikiwemo kugoma kupasha moto misuli katika mchezo wa Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich iliyopigwa Septemba 27.
Aidha mchezaji huyo amepewa muda wa siku 14 iwapo atahitaji kukata rufaa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.