Habari za Punde

*WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ATEMBELEA BANDA LA VODACOM KATIKA MAONYESHO YA BIDHAA ZA WAWEKEZAJI


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiangalia moderm ya intaenti ya kampuni ya Vodacom wakati Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo, Salum Mwalim akimpatia maelezo ya moderm hizo,wakati Waziri Mkuu alipotembelea banda la Vodacom katika maonyesho ya bidhaa na huduma pembezoni mwa mkutano wa wadau wa uwekezaji eneo la ziwa Tanganyika unaofanyika Mjini Mpanda. Mkutano huo utafunguliwa kesho Oktoba 17, na Rais Dk. Jakaya Kikwete.
 Meneja Mawasiliano wa kampuni ya Vodacom, Salum Mwalim akimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa SACP Isunto Mantage, wakati wawili hao walipokutana katika banda la Vodacom katika maonyesho ya wadau watakaoshiriki mkutano wa uwekezaji katika ukanda wa ziwa Tanganyika mjini Mpanda. Kampuni ya Vodacom imefadhili chakula cha mchana na cha usiku kwa wajumbe zaidi ya mia nne watakaohudhuria mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.