Habari za Punde

*YALIYOJILI PAMBANO LA MIYEYUSHO NA MATUMLA 'FULL ALBAM'

 Mabondia Issa Sewe wa Temeke (kulia) akichapana na Ramadhan Shauri wa Kinondoni, Sewe alishinda kwa Pointi ikiwa ni mmoja kati ya mapambano ya utangulizi wakati wa mapambano mawili ya Ubingwa, ambapo Kinondoni ilifanikiwa kutwaa mikanda yote.
 Ramadhan Shauri, akiwa hoi akitokwa na damu baada ya kuumizwa na mpinzani wake.
 Sehemu ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia mapambano hayo wakishangilia.
 Issa Sewe naye pia akiugulia maumivu akitokwa na damu baada ya kupata kipondo cha 'Rivange' kutoka kwa mpinzani wake, Shauri.
 Mgeni rasmi katika pambano hilo, Kamanda Kova, akifuatilia mapambano hayo ukumbini hapo.

HATIMAYE LILIKUJA PAMBANO LA MWAJUMA NDALA NDEFU NA ASHA NGEDELE
 Bondia Mwanadada kutoka mkoani Morogoro, Salma Kihobwa A.K.A 'Mwajuma Ndala Ndefu'  (kushoto) akimwadhibu mpinzani wake, Asha Nzoa wa Dar es Salaam, Asha Nzoa A.K.A Asha Ngedele, katika pambano lao la raundi 4.

Ndala Ndefu alishinda pambano hilo kwa Pointi. Pamoja na pambano hilo kuwavutia mashabiki waliokuwamo ukumbini humo lakini bado baadhi ya mashabiki walikelekea na kutoa maoni yao kwa Sufianimafoto kuwa iwapo kutakuwa na pambano jingine la wanadada siku nyingine basi waandaaji wajitahidi kuwaandalia mavazi yasiyowadhalilisha na si kama walivyovaa wadada hao.
Kama wanavyoonekana wanadada hao wakiwa na Singland ambapo mmoja wao alipata ngumi nzito hadi ziwa likatoka nje ya mikanda ya nguo hiyo wakati akijitahidi kujistili mwenzie aliendelea kumshambulia,
 Ndala Ndefu (kushoto) na Ngedele, wakiendelea kuchapana.
 Kichapo kinaendelea........
 Hatimaye Ndala Ndefu, alitangazwa mshindi wa pambano hilo.

PAMBANO LILILOISHA KATIKA RAUNDI YA KWANZA 'LAZIMA UKAE'
 Bondia wa Kinondoni (kushoto) akimwangalia kwa 'nyodo' mpinzani wake, wa TMK, baada ya kumpa konde zito lililompeleka chini katika raundi ya kwanza kati ya nane, ambapo mchezo ulimalizika katika raundi hiyo.
 Vibweka havikukosekana ndani ya ukumbi huo, huyu ni mtangazaji wa zamani wa kipindi cha watoto cha Redio One na ITV, Lulu, akiwa na kivazi cha hatari huku akipozi kwa picha baada ya kuona kamera ya Sufianimafoto akimdeku.
 Wadau wa mchezo huo wakiwa ukumbini humo na makocha wa mchezo huo.
 Bondia wa Kinondoni, Ramadhan Mashudu (kulia) akichapana na Mohammed Matumla. Matumla alishinda kwa Pointi.
 Baba akitoa maelekezo, Rashid Matumla akimpa maelekezo mwanae, wakati wa pambano hilo.
 Mashudu, akichapana na Matumla.

PAMBANO LA UBINGWA LA MADIA WA KINO NA FUNDI WA TMK
Bro mbona unaleta sifa utaniua mwenzio!!!
'Lazima Ukae' Fundi hatimaye alikalishwa na Majia.
 Aaah! wapi hiyo nimeiona..
 Hatimaye Majia wa Kino, alitangazwa mshindi na kuvishwa mkanda huo wa ubingwa uliokuwa ukishikiliwa na Fundi wa TMK.
 Majia alipongezwa na Kamanda Kova kwa ushindi huo.
 Mdada akipita kuonyesha Mknda wa Ubingwa wa UBO uliokuwa ukishikiliwa na Mbwana Matumla, wa TMK ambao naye pia akinyang'anywa na Miyeyusho wa Kino.
 Katika Raundi ya pili, Miyeyusho alikalishwa na Matumla kwa konde zito.
 Baada ya kupelekwa chini, Miyeyusho alihesabiwa hadi sita bila kuamka wala kuonyesha ishala ya kuendelea na pambano hilo jambo ambalo, liliwatia hofu mashabiki wake, kumbe alikuwa na hesabu zake, Saba, Nane, akainuka na kufuta Kisha.......
 Kilichofuata kilikuwa ni hiki, katika raundi hiyo hiyo, Miyeyusho alimshambulia Matumla kwa makonde ya haja, na hatimaje kumpeleka chini kama hivi, 'mijuu guuu'...............
 Matumla bado akijisikilizia chini kwanza, hukua akihesabiwa na mwamuzi.
 Baada ya hapo kichapo kiliendelea kwa zamu na sasa...........
 Matumla alizidiwa tena na kumdandia Miyeyusho wakati akielekea kwenda chini kwa mara ya pili.
 Kichapo kinaendelea....
 Matumla naye akafunguka lakini kilichofuata.......
 Matumla alipelekwa chini tena kwa mara ya tatu.......
 Alipoinuka naye akafunguka tena na kujitahidi kujibu mapigo lakini tayari alikwisha chelewa....ilikuwa ni raundi ya mwisho.
 Hatimaye Miyeyusho alitangazwa Bingwa mpya wa UBO na kuvishwa mkanda huo, hapa akihojiwa na waandishi wa habari, baada ya pambano hilo.



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.