Habari za Punde

*AKAUSHWA KAMA KUKU KWA IMANI ZA KISHIRIKINA IRINGA

UNYAMA GANI HUU JAMANI HADI LINI????? MTU mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Laurance Nkwera (60) mkazi wa Kijiji cha Ibani Ludewa katika Mkoa mpya wa Njombe, amekufa kwa kuchomwa moto na kuungua vibaya na watu wasiojulikana kwa imani za kishirikina, huku nyumba yake ikiteketezwa vibaya kwa moto, na familia yake kunusulika kifo kwa nyumba hiyo kutobolewa.

Ilizoeleka mambo haya kusikika zaidi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa sasa hata mikoa ya Kusini imeanza kufanya vitendo hivi vya kikatili, Sasa inabidi wahusika kuchukua hatua stahili ili kukomesha vitendo hivi. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.