Habari za Punde

*KIJITONYAMA SPORTS YACHUKUA FOMU KUSHIRIKI MASHINDANO YA KOMBE LA RANGERS

Mwandishi Wetu
TIMU ya soka ya Kijitonyama Stars Sports Club “Vijana Dozi Nene” ni miongoni mwa timu saba zilizochukua fomu kwa ajili ya kushiriki katika mashindano ya Kombe la Rangers yaliyopangwa kuanza mwezi ujao jijini.
Mratibu wa mashindano hayo, Abbas Ngau alisema kuwa mwisho wa kuchukua fomu kwa ajili ya kuthibitisha kushiriki ni kesho (Novemba) 20 na kuzitaka timu nyingine ambazo zinataka kushiriki katika mashindano ya mwaka huu kufanya hivyo kabla ya tarehe hiyo ya mwisho.
Ngau alisema kuwa Kijitonyama Stars Sports club inaungana na timu za Makumbusho Talent, Bodaboda ya Tandale, Swazi Inter, Small Jordan (Mwananyamala), Day Break (Magomen), Magic Power, ambazo zimepania kufanya kweli katika mashindano ya mwaka huu. Alisema kuwa jumla ya timu 20 tu zinatakiwa kushiriki katika mashindano ya mwaka huu.
Alisema kuwa mshindi wa kwanza wa mashindano hayo atazawadiwa sh. 300,000, jezi seti tatu na mipira mitatu wakati mshindi wa pili atapewa sh. 200,000, jezi seti mbili na mipira miwili na mshindi wa tatu atachukua sh. 100,000, jezi setu moja na mpira mmoja.
Mshindi wane katika mashindano hayo atazawadiwa sh. 50,000. Alisema kuwa sababu ya kuweka zawadi nono ni kurudisha hadhi ya mashindano hayo hasa baada ya kufanya uchaguzi wa viongozi wapya Oktoba 23 mwaka huu.

“Lengo ni kuwa na mashindano yenye msisimko mkubwa na kuwafanya wachezaji kuwa busy wakati wote wa msimu, hivyo tunaziomba timu zinazotaka kushiriki katika mashindano hayo kuja kuchukua fomu haraka,” alisema Ngau.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.