Habari za Punde

*MAITI YAZINDUKIA MOCHWARI MADAKTARI WAIPIMA WATHIBITISHA KIFO CHAKE

  Mgonjwa aliyezinduka akiwa Mochwari akihudumiwa na madaktari.
Na Francis Godwin, Iringa
MAUZAUZA ya amini usiamini yametokea mjini Iringa jana baada ya mgonjwa ambaye alifika kufanyiwa maombi kwa mmoja kati ya wahubiri maarufu mkoani Iringa kukata kauli akiwa nje ya ukumbi huo maarufu wa maombi na kuonyesha dalili zote za kuaga dunia jambo lililowafanya walioongozana naye kumpeleka kumuhifadhi katika  chumba cha kuhifadhia maiti (Mochwari) katika hospital ya mkoa wa Iringa.

Baada ya kufikishwa katika Chumba hicho maiti hiyo iliamka ghafla na kukaa ndipo wanandugu walipoamua kubeba mwili huo na kupeleka kwa madaktari kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mke wa mgonjwa huyo, Amina Ramadhan, alisema kuwa mume wake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria kwa kipindi cha mwezi mmoja sasa kabla ya jana mgonjwa huyo kuomba kuletwa mjini Iringa kwa mhubiri huyo maarufu mkoani Iringa, Boaz Sollo, wa kituo cha maombezi cha overcomers .

Hata hivyo alisema kuwa akiwa katika foleni ya kuingia ndani ya ukumbi ghafla mgonjwa huyo aliomba kupelekwa chooni na kabla ya kuingia chooni alikata kauli na hivyo kulazimika kuupeleka mwili wake mochwari katika hospital ya mkoa ambako kabla ya kuingizwa Mochwari ghafla marehemu aliamka na kuanza kurusha rusha mikono yake hali iliyopelekea kurudishwa tena mapokezi kwa ajili ya kuchunguzwa zaidi na kumtaja mjane wa marehemu Bi Amina Ramadhan alimtaja marehemu kuwa ni Gerald Tadei Ngusi.

Tukio hili limetokea majira ya saa 10 za jioni katika ukumbi huo wa IDYDC mjini Iringa madaktari walikwisha mpima na kuthibitisha kifo cha mgonjwa huyo.
 Wasamaliawema wakimshusha kutoka kwenye gari mgonjwa huyo 'marehemu' ili kumuingiza katika chumba cha matibabu baada ya kuzinduka akiwa Mochwari.
Wasamaria wema wakisimama nje ya chumba cha daktari kusubiri majibu huku mke wa marehemu akiwa amekaa chini.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.