Habari za Punde

*KAMATI KUU CCM 'YAMVUA GAMBA' KATIBU WA CCM MKOA WA DAR KILUMBE NGE'NDA

CHAMA cha Mapinduzi kupitia Mkutano wake wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ( NEC) imemtimua ama ‘Kumvua Gamba’ Kilumbe Ng’enda aliyekuwa Katibu wa Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kupatikana na  kosa la kwenda kinyume na maamuzi ya Vikao halali vya Chama hicho katika masuala ya Uchaguzi wa Madiwani wa Viti Maalum, ambapo sasa anasubiri kupangiwa kazi nyingine ndani ya Chama hicho.
Katika Hatua nyingine imegundulikwa kuwa baadhi ya watu waliokuwa wakihisiwa kuvuliwa Gamba katika maamuzi ya Kikao hicho, tayari walikwisha andaa makundi ya vijana ambao wangewapokea kwa nderemo na shangwe baada ya kutoka katika ukumbi huo na kuongozana nao kwa maandamano.
Na wengine tayari walikwisha andaaliwa sherehe na mapokezi makubwa huko katika makao yao na kufanyiwa mapokezi makubwa na mahasimu wakubwa wa CCM yaani CHADEMA, ambapo imeelezwa kuwa wangepokelewa na kukabidhiwa kadi za chama hicho.
Ikiwa hivyo ndivyo hivi kweli Mwanachma wa kweli anayekipenda chama chake kwa dhati na moyo mmoja wa kukitumikia kwa lengo la kuiletea Jamii faida na maendeleo makubwa pamoja na Taifa lake, kweli anaweza kubadilika ghfla kama Kintonga namna hiyo kweli ama ndiyo wale wanaokaa mahala kwa ajili ya Maslahi Fulani tu.
“Hii si sawa, kwani sidhani iwapo Baba yako Mzazi ataamua kukuadhibu kwa kulingana na kosa ulilotenda eti nawe ukaamua kumkana baba yako na kujipachika kwa ‘Jibaba’ jingine huku ukimkana Baba aliyekuleta Duniani na kukufanya ukaweza hata kufahamiana na hao ambao utawageuza kuwa baba mzazi,
Na kama unalengo la kweli katika kuhakikisha Chama chako kinaendelea kufanya vizuri na kujijengea heshima kwa wananchi wake ikiwa ni pamoja na kuwahudumia wananchi basi unapoonekana kwenda kinyume na maamuzi ama makubaliano ya Chama ukiwekwa pembeni huna haja ya kukasirika na kususa bali unatakiwa kutoa sapoti kwa yule anayekuja kuchukua nafasi yako na kukubaliana na matokeo.
Kwani hata timu za mpira wa miguu ni mfano tosha kabisa pale zinapokuwa mchezoni na kuamua kumfanyia mabadiliko mchezaji mmoja anayeonekana ama kuchoka ama kutocheza vizuri kwa siku hiyo ama kuumia, si kwamba anakuwa hajui la hasha ila anapopumzishwa anaweza kusoma mchezo ule na kujigundua makosa yake na katika mchezo ujao akipata nafasi ya kuanza tena hawezi kurejea makosa aliyoafanya katika mchezo uliopita” Hivi ndivyo nionavyo mimi. Sufianimafoto


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.