Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Asha Bilal, akisoma Hotuba yake wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Alliance Francaise Jijini Dar es Salaam Tanzania, iliyofanyika jana usiku kwenye Ukumbi wa Alliance Francaise Dar es Salaam. Katikati ni Balozi wa Ufaransa nchini, Marcel Escure (kushoto) ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Julia Giannetti.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Kikundi cha wake wa Mabalozi wa Nchi za Afrika, Mama Juma Khalfan Mpango, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Alliance Francaise Jijini Dar es Salaam Tanzania, iliyofanyika jana usiku kwenye Ukumbi wa Alliance Francaise Dar es Salaam. Kushoto ni Rahma Othman.
Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Julia Giannetti, akizungumza wakati wa sherehe hizo jana usiku.
Balozi wa Ufaransa nchini, Marcel Escure, akizungumza wakati wa hafla ya sherehe hizo.
Baadhi ya wadau wa Lugha ya Kifaransa waliohudhuria hafla hiyo, wakimsikiliza Mgeni rasmi Mama Asha Bilal, wakati akitoa Hotuba yake kwa Lugha ya Kifaransa.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Asha Bilal, akionyeshwa baadhi ya picha zilizowekwa katika ukumbi huo kwa ajili ya maonyesho ya maadhimisho hayo.
Kitanda kilichowekwa kwa ajili ya maonyesho katika Ukumbi huo kikiwa na hostoria ya pekee, ambapo shuka iliyotandikwa katika kitanda hicho imetengenezwa na Mwanadada kwa kutumia Bahasha za barua alizokuwa akiandikiwa na kutumiwa na Marafiki zake wa kiume tangu barua ya kwanza hadi ya mwisho wakati wa usichana wake wakati akiwa katika nchi mbalimbali duniani na kati ya hao ni wanaume 17 aliweza kutembea nao ambao nao pia amewaandika katika moja ya ua lake alilolifuma kwa mtindo wa kitambaa chini hapa.
Idadi ya wanaume aliopata kutembea nao mwanadada huyo kama alivyowaorodhesha.
No comments:
Post a Comment